Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, Katibu wa BAKWATA mkoa wa Dar es salaam alhaj Jamal Shao amewataka wachinjaji wanyama na ndege jijini Dar es salaam kuzingatia mafunzo maalum, maelekezo ya kitaalamu na kisheria yanayotolewa kwenye semina maalum ya siku mbili iliyofanyika BAKWATA Makao makuu, kwa sababu mafunzo na maelekezo hayo sasa ndiyo dira itakayotumiwa na wachinjaji kote nchini.
Alhaj Shao amesema hayo jana Jumamosi akifungua semina maalum na elekekezi ya wachinjaji kutoka machinjio ya Buguruni Ilala, Tegeta. Ukonga, Mbagala, Mtambani, Machinjio ya kisasa ya vingunguti na machinjio mengine Ambapo wataalanu mbalimbali wanatoa mafunzo kuwajengea uwezo wanjinjaji hao.
Alhja Shao amesema semina hiyo iliyoandaliwa na BAKWATA mkoa wa Dar es salaam inafuatia maelekezo ya Mufti wa Tanzania ambapo pia Mufti ameelekeza wachinjaji wote nchini wapewe vyeti na vitambulisho baada ya kupewa mafunzo hayo..
"Semina hii ya siku mbili inalenga kutoa mafunzo na maelekezo juu ya uchinjaji halali, haya ni mafunzo ya nadharia na vitendo, Mufti ameelekeza baada ya hapa wachinjaji wawe ni wale tu ambao wamepewa ujuzi, wamepimwa na kuonekana wanafaa ambao pia watapewa vyeti na vitambulisho vya uchinjaji halali." Amasema alhaj Shao.
Katibu huyo wa BAKWATA mkoa wa Dar es salaam amewataka makatibu wa BAKWARA kata na wilaya kutembelea machinjio yaliyo kwenye maeneo yao ili kutoacha mwanya kwa watu wasio na ujuzi kufanya kazi hiyo, amewataka makatibu hao kuchukua hatua stahiki kwa mtu yeyote anayechinja pasina kuzingatia taratibu za uchinjaji halali.
"Tunaishukuru serikali na tunaiomba iendelee kushirikiana nasi kuondoa machinjio na wachinjaji wasio rasmi ambao hawazingatii uchinjaji halali, kuchinja ni ibada na ni lazima ifanyike kwa kufuata misingi iliyoweka na Mwenyeezi Mungu Mtukufu ili kuwawezesha wale nyama halali" Amesema alhaj Shao.
Naye mmoja wa wachinjaji aliyejitambulisha kwa jina moja la Mikidadi ametoa shukurani za dhati kwa BAKWATA mkoa wa Dar es salaam na kusema semina hiyo ni muhimu na imekuja wakati muwafaka ambapo mashindano ya kikanda kibiashara yanazidi kushika kasi na njia ya kufaulu ni kuongeza ubora"
Kwa mujibu wa alhaj Shao semina hiyo imefungwa leo Jumapili jioni.
Maoni yako